Thursday 11 February 2010

Abdulrazak Gurnah


Najua itakuwa ngumu sana kwa vijana wa ulimwengu wa leo kumjua mtu huyu kutokana vijana kutofatilia kwa makini mambo kama haya hasa kwa wale ambao hawako mashuleni ama vyuoni
Hapa na mzungumzia Abdulrazak Gurnah ambaye ni mzaliwa wa Zanzibar,Gurnah amezaliwa mwaka 1948 katka kisiwa cha Zanzibar pwani ya Afrika mashariki,mwaka 1968 alienda Uk kama mwanafunzi ingawa safari yake hiyo ilikuwa ya utata sana kutokana na mazingira ya wakati huo hasa katika upande wa elimu kwani kwa wakati huo chuo ikikuu kilikuwa kimoja katika Afrika mashariki ambacho ni Makerere hivyo yeye aliamua kuvuka mipaka na kuelekea uingereza kwa lengo la kujiendeleza kielimu ambapo baada ya kumaliza kusoma alikuwa anafundisha katika chuo cha Kent.

Mbali ya kuwa alikuwa anafundisha lakini pia Gurnah ni mwandishim wa vitabu ambapo vitabu vyake vitatu vya kwanza ni memory of departure(1987), pilgrims away(1988) na dottie(1990),katika miaka yote aliyoishi uingereza hakuwahi kurudi nyumbani lakini baada ya miaka 20 alirudi Zanzibar kusalimia,Gurnah kwa sasa anaishi uingereza na ameoa .Amewahi kupata prize and award kwa kitabu chake itwacho paradise (1994),by the sea(2001).

No comments:

Post a Comment