Kwakweli huwa nasikia faraja sana pale ninapoona ama kusikia watu wanaishi na watu vizuri katika jamii inayowazunguka, kwanini nasema hivi!kwasababu kama nilivyosema kuwa mjue zaituni na lengo la kuanzisha blog hii ni kurekebisha tabia mbovu za baadhi ya watu ambao siku zote wao hawapendi kuona watu wanakuwa na maendeleo au maelewano na watu.
Naamini jambo hili halinikeri mimi tu hata wewe kama mpenda maendeleo lazima utachukia tabia kama hizi kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya watu,kukatisha tamaa na hata kupoteza malengo ya baadhi ya watu kutokana na msongo wa mawazo hasa pale yanapozidi hivyo kinachohitajika hapa ni kuwa makini sana na watu wa aina hiyo kwani wao wapo duniani kwa lengo moja tu kuharibu maisha ya watu kwasababu muda mwingine utakuta wanaingilia hadi mahusiano ya watu hivyo hawa ni watu wakuwaogopa sana na si wakuwafumbia macho hata kidogo.
Tuesday, 9 February 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment